Rasmi-Arsenal yatangaza kuingia mkataba Adidas

Arsenal leo imedhibitisha kuingia mkataba na kampuni ya Adidas kama mtengenezaji mkuu wa jezi za Arsenal kuanzia msimu ujao.

Rasmi-Arsenal yatangaza kuingia mkataba Adidas

Arsenal ilitangaza habari hizo kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter na bado hakuna taarifa za kina kuhusu mkataba huo ingawa taarifa tulizonazo ni kwamba mkataba huo ni mnono zaidi kuliko ule wa Puma uliosainiwa mwaka 2013 na unaisha tarehe 30 ya mwezi wa sita mwakani.


Mashabiki wengi wa Arsenal wameonesha kufurahishwa na taarifa hizo kwani kwa muda mrefu sasa puma wamekuwa wakitengeneza jezi ambazo mashabiki wengi wa Arsenal hawakuzipenda.

#COYG

Speak Your Mind

*