Rasmi-Bernd Leno ajiunga na Arsenal

Golikipa wa kijerumani  Bernd Leno amekubali kujiunga na Arsenal akitokea timu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Rasmi-Bernd Leno ajiunga na Arsenal

Golikipa mpya wa Arsenal Bernd Leno

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 ameichezea Bayer Leverkusen michezo zaidi ya 230 katika misimu saba aliyokuwa na timu hiyo ya kijerumani.

Alianza soka akiwa na timu ya  Stuttgart, Leno alijiunga na Leverkusen mwaka 2011 na mwaka huo huo mwezi wa tisa alikuwa aliweka rekodi ya kuwa golikipa mwenye umri mdogo zaidi kucheza katika ligi ya mabingwa wa ulaya akiwa na umri wa miaka 19 na siku 193, wakati timu yake ya Leverkusen ilipocheza na Chelsea katika hatua ya makundi.

Katika mechi za kimataifa,Bernd aliitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 na ameishaichezea timu hiyo katika michezo 6, mwaka jana alikuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa kombe la mabara.

Baada ya kukamilika kwa usajili huo kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery alisema “Tumefurahi ya kwamba Bernd Leno amejiunga nasi, amekuwa akicheza kwa kiwango kwa juu na kuwa kipa wa kwanza wa Leverkusen kwa muda mrefu katika ligi kuu ya Ujerumani katika miaka 7 iliyopita.Wote tuna furaha kubwa ya kwamba Bernd amechagua kujiunga na timu ya Arsenal, na tunategemea kuanza kufanya naye kazi wakati wa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya ”.

Kipa huyo mpya bado hajapewa namba,ambayo itatangazwa muda mfupi ujao.

Karibu Arsenal Bernd Leno

Je unauonaje usajili huu? tupia maoni yako hapa chini.

Speak Your Mind

*