Rasmi-Sokratis Papastathopoulos ajiunga na Arsenal

Arsenal imekamilisha usajili wa beki wa kigiriki  Sokratis Papastathopoulos kutoka katika timu ya  Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekwa hadharani.

Rasmi-Sokratis Papastathopoulos ajiunga na Arsenal

Kupitia tovuti rasmi ya timu, Arsenal wametangaza usajili wa beki wa kigiriki Sokratis Papastathopoulos kutoka Dortumund.

Beki huyo wa kati amesaini mkataba wa muda mrefu wa kuichezea Arsenal ingawa hawajaweka wazi ni kiasi gani atalipwa na pia hakuna taarifa rasmi ya kwamba amesajiliwa kwa dau la kiasi gani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ameishaichezea timu ya taifa ya Ugiriki katika michezo 79 na katika miaka mitano iliyopita aliichezea timu hiyo ya Ujerumani katika michezo 130 ya ligi ambapo alifunga magoli saba.

Mchezaji huyo anakuwa mchezaji wa tatu kusajiiwa na Arsenal msimu huu baada ya kusajiliwa kwa  Stephan Lichtsteiner kutoka  Juventus, na kipa  Bernd Leno, kutoka  Bayer Leverkusen.

Sokratis  atavaa jezi namba 5 ndani ya Arsenal, Arsenal itacheza mchezo wake wa kwanza wa ushindani kwenye ligi dhidi ya Manchester City wikiendi ya tarehe 11-12 mwezi wa nane.

Karibu Socratis

Je mashabiki wa arsenal mnauonaje usajili huu? unakidhi mahitaji ya timu ama bado? tupia maoni yake hapa chini.

 

Comments

  1. Lubekano Aluba Karl says

    Timu kwa sasa, inaleta matumaini kwa upande wa beki kwa sababu msimu uliopita, timu imefungwa goli nyingi kutokana na uzembe wa mabeki pamoja na Goal Keeper. Nina matumaini makubwa sana kwa usajili huo. Na uzuri ni kwamba coach hatumii longolongo za maneno sana kwani akisudia anatimiza.

Speak Your Mind

*