Raul Sanllehi Afutiwa mkataba na Arsenal

Timu ya ArsenalĀ  imesitisha mkataba na aliyekuwa mkurugenzi wa soka wa timu hiyo Raul Sanllehi na nafasi yake itachukuliwa na mkurugenzi mwandamizi wa timu hiyo Vinai Venkatesham.

Raul Sanllehi Afutiwa mkataba  na Arsenal

Katika taarifa rasmi katika mtandao wa Arsenal, inaonesha ya kwamba uamuzi huo umefikiwa kwa pamoja kati ya timu na Raul.

Kufutiwa mkataka kwa Raul kunafuatia tetesi zilizozuka juzi za kwamba Arsenal ilikuwa inachunguza usajili wa Pepe kwani timu ilitumia pesa nyingi mno kukamilisha usajili huo na Raul alikuwa mhusika mkuu katika usajili huo.

Kupitia ukurasa rasmi wa timu, mmiliki wa Arsenal, Stan Kroenke, alimshukuru Raul kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa Arsenal katika miaka mitatu kama mtumishi wa Arsenal.

Raul pia alitumia ukurasa huo kuwashukuru viongozi wa Arsenal, ambapo alisema ya kwamba anajisikia faraja kubwa kufanya kazi katika timu kubwa kama Arsenal na atachukua muda huu kupumzika yeye na familia yake.

Bado haijajulikana ni nini sababu kubwa ya kufanya mabadiliko hayo hasa katika kipindi hiki cha usajili, naamini katika siku chache zijazo tutapata taarifa rasmi.

Kila la heri Don Raul

Tupia Maoni Yako Hapo Chini