Salah-Eddine ajiunga na Arsenal

Salah-Eddine ajiunga na Arsenal

Timu ya Arsenal imekamilisha usajili wa mchezaji kinda Salah-Eddine kutoka katika timu ya Feyenoord ya Uholanzi.

Salah-Eddine ambaye anajulikana zaidi kama Salah ni mchezaji mwenye umri wa miaka 17 amejiunga na Arsenal bure, kwa sasa atakuwa katika kikosi cha vijana cha Arsenal.

Salah anayeimudu vyema nafasi ya kiungo wa kati anasikifa zaidi kwa uwezo wake wa kupiga pasi na kutengeneza magoli kutoka katikati ya uwanja.

Salah ameanzia maisha yake ya soka nchini uholanzi, amekulia mjini Rotterdam, ambapo amezichezea timu mbali mbali za vijana za Feyenoord.

Usajili huo ni mwendelezo wa Arsenal wa kukusanya wachezaji vijana wenye vipaji wa gharama ndogo na kuwatunza ili ikiwezekana baadaye waichezee timu ya wakubwa ama kuwauza kwa faida.

Salah anajuwa mchezaji wa nne wa timu ya vijana kusajiliwa ndani ya wiki mbili zilizopita.

Tupia Maoni Yako Hapo Chini