Tetesi-Arsenal kumsajili Gary Cahill siku ya mwaka mpya

Makampuni mengi ya upatu yanaipa nafasi kubwa Arsenal ya kumsajili beki wa kati wa Chelsea,Gary Cahill ifikapo tarehe moja ya mwezi wa kwanza 2019.

Tetesi-Arsenal kumsajili Gary Cahill siku ya mwaka mpya

Gary Cahill ambaye amekosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea chini ya kocha muitaliano Mauricio Sarri inasemekana amechoka na hali hiyo na yupo tayari kuhama, pia inasemekana ya kwamba kocha Sarri naye yupo tayari kumuuza iwapo itapatikana timu inayomuhitaji.

Baada ya kuumia kwa Rob Holding na Laurent Koscienly kutokuwa fiti kimchezo taarifa tulizonazo ni kwamba Arsenal ipo sokoni kutafuta beki wa kati ambaye ataziba pengo hilo.

Mabeki wa kati waliohusishwa na kuhamia Arsenal ni Fernando Calero, Erick Bailly na sasa Gary Cahil, Calero alionekana London jumapili iliyopita na kuzua tetesi za kwamba yupo mbioni kujiunga na Arsenal.

Kampuni ya upatu ya Ladbrokes inpokea beti za 7/4 ya kwamba Cahil atahamia Arsenal tarehe moja ya mwezi ujao.

Je kati Fernando Calero, Erick Bailly na Gary Cahil yupi ungependa aje Arsenal? tupia maoni yako hapa chini

Speak Your Mind

*