Tetesi-Arsenal kuwauza Danny Welbeck, David Ospina na wachezaji wengine

Wakati Arsenal ikiendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi na michezo mingine, kuna tetesi za kwamba Arsenal ina mpango wa kuwauza wachezaji kadhaa wakiwemo Danny Welbeck na David Ospina ili kupunguza ukubwa wa kikosi.

Tetesi-Arsenal kuwauza Danny Welbeck, David Ospina na wachezaji wengine

Mpaka sasa Arsenal ilikuwa imeelekeza nguvu zake katika kusajili wachezaji wapya na tayari imeshatumia paundi milioni 70 ili kupata saini za wachezaji Bernd LenoSokratis PapastathopoulosLucas TorreiraStephan Lichtsteiner na Matteo Guendouzi.

Sasa Arsenal imehamishia nguvu zake katika kuwauza wachezaji ili kupunguza ukubwa wa kikosi na pia kupata pesa kwa ajili ya mishahara na usajili wa wachezaji wapya.

Mtandao wa The Telegraph unahabarisha ya kwamba mshambuliaji Danny Welbeck na kipa namba tatu David Ospina ni miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa kuondoka Arsenal katika dirisha hili la usajili.

Wachezaji hao inasemekana hawapo kwenye mipango ya kocha Unai Emery, pia wachezaji kama Lucas Perez, Carl Jenkinson,Chuba Akpom na Joel Campbell wanaweza kuuzwa ili kutengeneza pesa za usajili wa wachezaji wapya.

Welbeck anaingia katika mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake na Arsenal na Ospina kwa sasa ni chaguo la tatu baada ya Leo na Petr Cech.

Je ungependa mchezaji gani aondoke na nani abaki? tupia maoni yako hapa chini.

Speak Your Mind

*