Tetesi-Arsenal wanampango wa kusajili Eric Bailly

Kuna taarifa za kwamba Arsenal wana mpango wa kumsajili beki wa Manchester United Eric Bailly, hii ni kwa mujibu wa gazeti la The Guardian.

Tetesi-Arsenal wanampango wa kusajili Eric Bailly

Eric Bailly ambaye alikuwa ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha wa Manchester United Jose Mourinho kwa dau la paundi milioni 30, inasemekana ni mmoja ya wachezaji ambao hawaivi na kocha huyo kwa sasa na anaweza akatupiwa vilago vyake katika dirisha la usajili la mwezi wa kwanza.

Katika taarifa nyingine tulizopata ni kwamba Manchester United wanataka kumtumia mchezaji huyo kama chambo cha kumpata nyota wa Arsenal Aaron Ramsey mwezi wa kwanza.

Eric Bailly alinunuliwa kwa paundi 30 mwaka 2916 na kuna tetesi za kwamba Arsenal wapo tayari kumuachia Ramsey mwezi wa kwanza kwa paundi milioni 25, hivyo Manchester United wanaona ya kwamba wanaweza kubadilishana wachezaji hao.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Arsenal na Manchester United kubadilishana wachezaji kwani walifanya hivyo kwa Alexis Sanchez na Henrik Mkhitaryan.

Binafsi sioni sababu ya Arsenal kumsajili Eric Bailly kwani ni beki anayetumia nguvu zaidi kuliko akili, hana uwezo wa kupiga pasi hivyo hataweza kumudu mfumo wa Arsenal ambapo wanapiga pasi kutokea kwa kipa.

Je wewe unasemaje kuhusu tetesi hizi? tupia maoni yako hapa chini.

Speak Your Mind

*