Tetesi-Arsenal Waulizia kuhusu Thiago Alcantara

Kituo cha luninga cha ESPN kinahabarisha ya kwamba Arsenal imewasiliana na timu ya Bayern Munich kwa nia ya kumsajili kiungo wa timu hiyo Thiago Alcantara.

Thiago Alcantara

 

Taarifa hizo zinaeleza ya kwamba Bayern Munich wana mpango wa kumuuza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 kwani amebakisha mwaka mmoja tu katika mkataba wake.

Bayern Munich ipo tayari kumuachia mchezaji huyo kwa dau la paundi milioni 23 lakini Arsenal ina mpango wa kuongea na timu ya Bayern Munich ili wapunguziwe kwani mchezaji huyo atataka kulipwa mshahara mkubwa.

Inaaminika ya kwamba Liverpool ndiyo waliokuwa katika nafasi ya kwanza katika mbio za kumsajili beki huyo, lakini kuingia kwa Arsenal katika mbio hizo kunabadilisha kila kitu kwani mchezaji huyo ana uhusuano mzuri na kocha mkuu wa Arsenal Mikel Arteta.

Iwapo Arsenal itafanikiwa kukamilisha mpango wa kumsajili  Thiago Alcantara, utakuwa ni moja ya sajili bora kabisa kwani kwa mtazamo wangu, timu kwa sasa haina kiungo hata mmoja anayefikia kiwango cha mchezaji huyo.

 

 

Tupia Maoni Yako Hapo Chini