Tetesi, Arsenal yakamilisha usajili wa kinda la PSG Yacine Adli

Kocha mpya wa Arsenal, Unai Emery anaendelea na mipango yake ya kuijenga upya timu hiyo baada ya kuwepo na taarifa ya kwamba tayari ameshakamilisha usajili wa mchezaji mwingine kutoka PSG Yacine Adli.

Tetesi, Arsenal yakamilisha usajili wa kinda la PSG Yacine Adli

Baada ya jana kutangaza rasmi usajili wa beki wa kulia Stephan Lichtsteiner na kukiwa na tetesi za kwamba tayari usajili wa beki wa kati Socratis nao umekamilika,inaelekea kocha huyo ameamua kumchukua kinda huyo ili kuimalisha safu ya kiungo.

Katika taarifa iliyoandikwa na mitandao mingi na kuthibitishwa na mtandao wa goal.com. Arsenal imekamilisha usajili wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17.Ili kukamilisha usajili huo Arsenal imeilipa PSG fidia ya paundi  £223,000.

Inasemekana Yacine Adli alikataa mkataba mpya na PSG baada ya kushawishiwa na Emery na Mislitant ya kwamba ana nafasi kubwa zaidi ya kufanya vizuri Arsenal kuliko akibaki Ufaransa.

Adli, amesaini mkataba wa miaka mitatu na iwapo atafanya vizuri ataongezewa miaka mingine miwili na kuufanya mkataba huo kuwa wa miaka mitano.

Mchezaji huo anayecheza kama kiungo mshambuliaji na pia kama winga wa kulia ameishazichezea timu za vijana za Ufaransa za umri wa mika 16, 17 na 18, ambapo amefunga magoli 13 katika michezo 23 aliyozichezea timu hizo za taifa.

Je unauonaje usajili wa dogo huyo tupia maoni yako hapa chini.

Comments

  1. Abel ikomeja says

    Well for arsenal to get a new player it so nice for me

Speak Your Mind

*