Tetesi-Arsenal yakubaliana na Fiorentina kuhusu usajili wa Lucas Torreira

Kiungo wa Arsenal, Lucas Torreira yupo mbioni kujiunga na timu ya Fiorentina ya Italia baada ya timu hizo  kufikia makubaliano juu ya uhamisho wa mchezaji huyo.

Tetesi-Arsenal yakubaliana na Fiorentina kuhusu usajili wa Lucas Torreira

Katika taarifa tulizozipata ni kwamba Arsenal na Fiorentina tayari wamekubaliana ada ya uhamisho wa mkopo kwa dau la paundi milioni 7.3 na ada ya uhamisho ya paundi milioni 14 katika usajili ujao wa majira ya joto.

Arsenal walimsajili Torreria kwa dau la paundi milioni 27 kutokea timu ya Sampdoria ya Italia lakini kutokana na hali ya uchumi ya timu nyingi kuyumba wameshindwa kupata timu iliyotayari kuwarudishia kiasi hicho cha pesa.

Kiungo huyo raia wa Uruguay alijiunga na Arsenal miaka miwili iliyopita, mwaka wa kwanza alifanya vizuri sana, lakini mwaka wa pili aliyekuwa kocha wa Arsenal Unai Emery aliamua kumchezesha mchezaji huyo kama kiungo mshambuliaji hali iliyosababisha kiwango cha mchezaji huyo kuporomoka kwa kasi sana.

Baada ya Unai kuondoka na kuja kwa Mikel Arteta mchezaji huyo alianza katika kikosi cha kwanza katika mfumo wa 4-2-3-1 akicheza kiungo na Granit Xhaka.

Alifanikiwa kucheza michezo michache katika kikosi cha kwanza kabla ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Dani Ceballos.

Kuongezeka kwa maelewano kati ya Dani Ceballos, mabadiliko ya mfumo na kushindwa kurudia kiwango chake cha awali vilimfanya Torreira aendelee kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza baada ya kupona.

Tupia Maoni Yako Hapo Chini