Tetesi-Barcelona wanataka kubadilishana Dembele na Aaron Ramsey

Barcelona wapo tayari kumuachia Ousmane Dembele ajiunge na Arsenal kwa sharti moja tu, Arsenal iwape Aaron Ramsey.

Tetesi-Barcelona wanataka kubadilishana Dembele na Aaron Ramsey

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amehusishwa na kuhamia Arsenal mara nyingi katika dirisha hili la usajili na kuna tetesi za kwamba Barcelona hawamtaki hasa baada ya kumsajili Malcom siku chache zilizopita.

Gazeti la The Sun  linadai ya kwamba Arsenal wanaweza kulazimishwa kumuachia Ramsey kama wanataka kumpata kinda huyo kutoka Barcelona.

Mpaka sasa Arsenal imeshasajili wachezaji watano na kuna habari za kwamba wana mpango wa kusajili mchezaji mmoja ama wawili ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji hasa upande wa mawinga.

Arsenal itabidi ifanye kazi ya ziada ili kumsajili Dembele ambaye kwa sasa ni mchezaji wa tatu kwa kununuliwa kwa bei kubwa duniani, kwani Barcelona walilipa pesa nyingi ili kumsajili mwaka mmoja uliopita na watataka kurudisha sehemu kubwa ya pesa hizo.

Dembele,ambaye alisajiliwa kwenda kwa wakali hao wanaotumia uwanja wa  Nou Camp  kwa dau la paundi milioni 134 ameshindwa kuwika akiwa na timu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alifanikiwa kufunga magoli matatu tu katika ligi kuu ya Hispania msimu ulioisha.

Na Barcelona wapo tayari kumuuza, lakini wanamtaka Aaron Ramsey kama sehemu ya usajili huo,Ramsey anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa sasa na iwapo asiposaini sasa anaweza kuondoka bure mwakani.

Je mashabiki wa Arsenal, mnaonaje tetesi hizi? wabadilishane au kila mtu abakie na wake?

Comments

  1. Wabadilishe,sasa nember 6 mwengine kama huyo atatoka wapi?

Speak Your Mind

*