Tetesi-Chelsea wakubali kumuuza David Luiz kwenda Arsenal

Wakati leo ni siku ya mwisho wa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi, kumezuka tetezi za kwamba Chelsea ipo tayari kumuuza beki wake wa kati David Luiz kwenda Arsenal.

Tetesi-Chelsea wakubali kumuuza David Luiz kwenda Arsenal

Baada ya kumuuza nahodha wake Laurent Koscienly,Arsenal ipo sokoni kutafuta beki mpya wa kati na imehisishwa na uhamisho wa mabeki wengi wa kati, lakini katika hali ambayo haikutarajiwa usiku wa kuamkia leo zimeibuka tetesi za kwamba David Luiz jana hakufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Chelsea katika kujaribu kulazimisha uhamisho huo na masaa machache baadaye zikaibuka tetesi zingine za kwamba Chelsea ipo tayari kumuuza beki huyo.

Taarifa hizo zilizoandikwa na vyombo vingi vya habari vya kiingeleza zinadai ya kwamba mchezaji huyo amekuwa hana furaha ndani ya timu hiyo kutokana na kuwa na imani ya kwamba hayumo katika mipango ya  kocha mkuu wa Chelsea, Frank Lampard.

Kama Arsenal watakamilisha usajili huo, binafsi sioni tatizo kubwa kwani David Luiz ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa atasaidia kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi kwa mwaka mmoja wakati Arsenal ikisubiri ujio wa Wiliam Saliba.

Je wewe unauonaje usajili huo ? tupia maoni yako hapa chini.

Speak Your Mind

*