Tetesi-EMILE SMITH ROWE AKARIBIA KUTUA RB LEIPZIG KWA MKOPO

Tetesi-EMILE SMITH ROWE AKARIBIA KUTUA RB LEIPZIG KWA MKOPO

Mchezaji kinda wa Arsenal, Emile Smith Rowe anakaribia kujiunga na timu ya RB Leipzig kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Mtandao wa Sky Sports umeandika kwenye ukurasa wao ya kwamba mpango huo wa kumtoa Smith Rowe kwa mkopo umetokana na Arsenal na Arsenal kukamilisha usajili wa Denis Suarez kutoka Barcelona (tunaamini usajili huo umekamilika ila bado sio rasmi kutoka timu ya Arsenal) na pia kuna uwezekano wa Carasco kutua hivyo wameona ya kwamba ni bora aende kwa mkopo ili apate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Taarifa hizo zinaendelea kuhabarisha ya kwamba mchezaji huyo atasafiri mapema kesho kwenda Ujerumani kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na kusaini mkataba wa kujiunga na timu hiyo.

Smith Rowe ambaye amecheza vizuri katika michezo yote aliyoichezea Arsenal msimu huu anachukuliwa kama mmoja ya vipaji bora kabisa kuwahi kuzalishwa na Arsenal katika miaka ya karibuni.

Leave a Reply

avatar
  Subscribe  
Notify of