Tetesi-Fernando Calero aonekana London

Beki wa kati wa timu ya Real Valladolid ya Hispania, Fernando Calero ameonekana mjini London na kuibua tetesi za kwamba yupo mbioni kujiunga na Arsenal.

Tetesi-Fernando Calero aonekana London

Fernando Calero (pichani juu) amehusishwa na kuhamia Arsenal

Sio siri ya kwamba Arsenal wapo sokoni wakitafuta beki wa kati baada ya Rob Holding kuumia na atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 9, Laurent Koscienly bado hajapona vizuri baada ya kuumia kifundo cha mguu mwezi wa tano mwaka huu.

Kutokana na tatizo la majeruhi ambapo mabeki wote ni majeruhi, kocha mkuu Unai Emery amelazimika kumtumia Granit Xhaka ambaye ni kiungo mchezeshaji kama beki wa kati hali inayoifanya timu kukosa mtu wa kuanzisha mashambulizi.

Calero ambaye ana umri wa miaka 23 ana kipengele kinachomruhusu kuhama timu hiyo kwa dau la paundi milioni 10 na inasemekana ya kwamba Arsenal wapo tayari kutoa kiasi hicho cha pesa.

Mchezaji huyo aliongozea moto katika tetesi hizo baada ya kuweka picha jumapili usiku baada ya kuweka picha akiwa London Waterloo kwenye mtandao wa Instagram.

calero akiwa london

Je ungependa Fernando Calero atue Arsenal ? tupia maoni yako hapa chini.

Speak Your Mind

*