Tetesi-Juan Mata kujiunga na Arsenal msimu ujao

Mtandao wa TalkSport umeandika ya kwamba mchezaji Juan Mata atajiunga na Arsenal msimu ujao baada ya kumaliza mkataba wake na Manchester United.

Tetesi-Juan Mata kujiunga na Arsenal msimu ujao

Juan Mata yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na kuna taarifa ya kwamba Man United bado hawajaanza mazungumzo ya kumpatia mkataba mpya.

Mata alicheza chini ya kocha wa wa Arsenal Unai Emery kwa miaka mitatu wakiwa na timu ya Valencia ya Hispania na katika kipindi hicho alifanikiwa kuingia katika timu ya taifa ya Hispania na baadaye kuhamia Chelsea.

Ni rahisi kugundua ya kwamba Mata sio chaguo la Mourinho kwani baada ya kurudi Chelsea kocha huyo alimuuza kiungo huyo kwa Manchester United.

Na sasa inaonekana ya kwamba kocha huyo yupo tayari kumuachia mchezaji huyo baada ya kugoma kumpa mkataba mpya na vyombo vya habari vinaanza kutunga tetesi za kuhamia Arsenal.

Juan Mata ana miaka 30, yupo katika mkataba mkubwa na Manchester United, sidhani kama kwa kiwango chake cha sasa anaweza akawa msaada kwa timu na pia sidhani kama Arsenal watakuwa tayari kumpa mshahara mkubwa mchezaji ambaye atakuwa hayupo katika kikosi cha kwanza.

Pia ikumbukwe ya kwamba Arsenal hawana bahati sana na wachezaji kutoka Man United, mchezaji wa mwisho kuhamia Arsenal kutokea timu hiyo ni Henrik Mkhitryan ambaye kwa mtazamo wangu hajaonesha kiwango kikubwa tangu atue mwezi wa kwanza mwaka huu.

Je wewe unasemaje kuhusu tetesi hizi? toa maoni yako hapa chini.

Speak Your Mind

*