Tetesi-Mesut Özil kuuzwa kwa paundi milioni 25 tu

Wakati dirisha dogo la usajili likikaribia, kuna tetesi za kwamba Arsenal ipo tayari kumuuza kiungo wake mshambuliaji Mesut Özil kwa dau la paundi milioni 25 tu.

Tetesi-Mesut Özil kuuzwa kwa paundi milioni 25 tu

Mitandao mingi ya habari, ukiwamo wa Daily Mail imeandika ya kwamba Arsenal ipo tayari kumuuza kwa hasara kiungo huyo kwani wanaona ya kwamba mshahara anaopata kwa paundi 350,000 kwa wiki ni mkubwa mno kulinganisha na mchango wake kwenye timu na wanaona wanaweza kupata mbadala wake kwa nusu ya mshahara huo.

Ikumbukwe ya kwamba Mesut Özil hajaichezea Arsenal katika michezo mitano iliyopita kwa madai ya kwamba alikuwa na maumivu ya mgongo.

Taarifa hizo zinaendelea kudai ya kwamba Inter Milan ipo tayari kutoa dau hilo ili kumpata kiungo huyo na kwamba maongezi kati wa wakala wa Özil na timu hiyo yataanza wiki ijayo.

Mtazamo wangu

Kwa upande mmoja vigumu kuamini tetesi hizo kwani hawajasema ni wapi wamezitoa habari hizo, lakini kwa upande mwingine naona mwisho wa Mesut Özil ndani ya Arsenal unakaribia kwani amekuwa akikosa mechi nyingi kuanzia mwishoni mwa msimu uliopita na siamini kama uongozi mpya wa Arsenal utaweza kumvumilia.

Pia naamini ya kwamba litakuwa kosa kubwa sana kumuuza Mesut Özil bila ya kusajili mchezaji atakayeziba pengo lake kwani kwa sasa hakuna kiungo mshambuliaji wa kuaminika na mwenye uwezo wa kutengeneza nafasi kama yeye ndani ya kikosi hiki cha Arsenal.

Mfano mzuri ni katika mchezo wa jana ambapo mwalimu Unai Emery alilazimika kuwaanzisha viungo wakabaji watatu, pia Iwobi na Mkhi leo wanacheza vizuri kesho wanacheza chini ya kiwango, sio wa kuwaamini sana.

Je wewe unasemani, unataka Mesut Özil auzwe na aletwe mchezaji mwingine au aendelee kukipita katika timu ya Arsenal, tupia maoni yako hapo chini.

Speak Your Mind

*