Tetesi za usajili Arsenal-Andre Gomes-Dembele na Pavon

Wakati Arsenal ikiendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya,magazeti mengi yameendelea kuihusisha na usajili wa wachezaji mbali mbali, leo tunakuletea tetesi za usajili zinazowahusu wachezaji Andre Gomes,Dembele na Pavon.

Andre Gomes

Arsenal imeanza mazungumzo na Barcelona kuhusu usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Ureno,Andre Gomez.Katika taarifa zilizoandikwa na vyombo mbali mbali vya habari mchezaji huyo amepania kuachana na timu hiyo ya Hispania kutokana na kukosa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Mtandao wa Paris United umeandika ya kwamba Arsenal wameshawasiliana na mchezaji huyo na Barcelona wapo tayari kumuachia mchezaji huyo.

Cristian Pavon

Kocha wa Arsenal,Unai Emery ameambiwa kiasi cha pesa ambacho anatakiwa kulipa kama anamtaka mchezaji Cristian Pavon kutoka Boca Juniors.

Gazeti la Daily Mirror linaandika ya kwamba mchezaji huyo amesaini mkataba mpya na Boca na kuna kipengele kinachomruhusu mchezaji huyo kwa dau la paundi milioni 44.

Dembele awapagawisha mashabiki wa Arsenal

Tetesi za usajili Arsenal-Andre Gomes-Dembele na Pavon

Ousmane Dembele

Kwa muda sasa Arsenal imekuwa ikihusishwa na usajili wa Ousmane Dembele kutoka Barcelona,mchezaji huyo ambaye hakucheza vizuri msimu uliopita alikuwa ni sehemu ya timu ya taifa ya Ufaransa iliyoshinda kombe la Dunia jana.

Kilichotokea ni kwamba mchezaji huyo alikoment katika picha ya beki mpya wa Arsenal Sokratis ambapo alisema ‘big papa’.

Kitendo hicho kimewafanya mashabiki wengi wa Arsenal waamini ya kwamba mchezaji huyo yupo njiani kutua Arsenal.

Pia wiki iliyopita Aubamayang aliweka picha ya Dembele katika mtandao wa instagram hali ambayo pia iliibua tetesi za kwamba huenda mchezaji huyo akatua Arsenal.

Hizo ndizo tetesi za usajili wa Arsenal tulizozipata kwa leo, zingine kesho tukijaaliwa.

Speak Your Mind

*