Tetesi za usajili Arsenal-Chuky Lozano na Hector Herrera wanatakiwa na Arsenal

Habari kutoka Mexico zinadai ya kwamba Arsenal ina mpango wa kuwasajili Chuky Lozano na Hector Herrera katika dirisha hili la usajili.

Kituo cha luninga cha ESPN Mexico jana jioni kilitoa taarifa ya kwamba wachezaji hao wawili wanatakiwa na timu ya Arsenal.

Chuky Lozano

Tetesi za usajili Arsenal-Chuky Lozano na  Hector Herrera wanatakiwa na Arsenal

Chuky Lozano

Hirving Lozano ambaye kwa hapa Mexico anajulina kama Chucky Lozano amekuwa akiwindwa na timu kubwa za Ulaya na katika taarifa hizo inasemekana Arsenal ni moja ya timu hizo, taarifa hiyo inaenda mbali zaidi na kusema ya kwamba tayari Arsenal wameshakutana na wawakilishi wa mchezaji huyo na wapo tayari kutoa dau la paundi milioni 35 ili kumsajili mchezaji huyo ambaye kwa sasa anaichezea timu ya PSV ya Uholanzi.

Hector Herrera

Hector Herrera

Hector Herrera

Pia taarifa hizo zinaelezea ya kwamba Arsenal inataka kumsajili mchezaji wa kiungo wa Mexico Hector Herrera ambaye Mexico ni maarufu kama HH.

Herrera ambaye ni kiungo mkabaji kwa sasa anaichezea timu ya Porto ya Ureno,kwa mujibu wa taarifa hiyo usajili wa Hector Herrera utategemea sana na kukamilika kwa usajili wa mchezaji Lucas Torreira kutoka Sampdoria, kwani Herrera atasajiliwa tu iwapo kama Arsenal itamkosa Lucas Torreira.

Mimi binafsi ningependa Chuky Lozano achezee Arsenal kwani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ni mmoja ya wachezaji ambao ndani ya miaka 2 au 3 wanaweza kuwa bora kabisa duniani.

Speak Your Mind

*