Tetesi za usajili Arsenal-Kingsley Coman-N’Zonzi na Golovin

Arsenal inaendelea na kujiandaa na msimu ujao wa ligi ambapo jana ilicheza na timu ya Crawley town na kuifunga goli 9-0,na wiki iliyopita kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery, alisema ya kwamba kikosi chake kimekamilika.

Lakini kutokana na kuwa katika kipindi cha usajili bado Arsenal inahisishwa na kusajili wachezaji wapya.Katika tetesi za usajili leo tunakuletea habari zilizoandikwa na magazeti kuhusu wachezaji Kingsley Coman ,N’Zonzi na Golovin ambao wamehusishwa na usajili wa Arsenal.

Kingsley Coman

Tetesi za usajili Arsenal-Kingsley Coman-N'Zonzi na Golovin

Kingsley Coman

Arsenal imekuwa ikihusishwa na uhamisho wa mchezaji Kingsley Coman kutoka Bayern Munich na kulikuwa na tetesi ya kwamba Arsenal walituma ofa ya paundi milioni 50 ambayo ilikataliwa na wakarudi tena na ofa ya paundi milioni 55 ambayo ilikataliwa pia.

Sababu kubwa ya Bayern Munich kuzikataa ofa za Arsenal ni kuwa wanamuona mchezaji huyo kama sehemu kubwa ya safu yake ya ushambuliaji hasa ukichukulia wachezaji kama Frank Ribery umri umeshawatupa mkono na Kingsley Coman atachukua nafasi yake siku si nyingi.

Steven N’Zonzi

Steven N’Zonzi

Steven N’Zonzi

Kituo cha Sky Sports kimeandika katika tovuti yake ya kwamba Arsenal wanaendelea mazungumzo na Sevilla kuhusu uwezekano wa kumsajili mchezaji Steven N’Zonzi. Mchezaji huyo ambaye amewahi kufanya kazi na Unai Emery anaweza kucheza kama kiungo mkabaji na anaweza kuja kuongeza nguvu katika kiungo cha Arsenal.

Aleksandr Golovin

Arsenal ilikuwa inamtaka Aleksandr Golovin, na Arsenal inaelekea kumkosa mchezaji huyo ambaye ameamua kujiunga na Chelsea.

Inasemekana ya kwamba mchezaji huyo alikuwa tayari kujiunga na Arsenal lakini baada ya Arsene Wenger kuondoka Arsenal ameamua kubadili uamuzi wake kwani alikuwa ni shabiki mkubwa wa kocha Wenger.

Hizo ndizo tetesi za usajili za Arsenal tulizozipata kwa siku ya leo,usisahau kushare na mashabiki wengine wa Arsenal.

Comments

  1. Am Real Arsenal Fans, I Need More Detail About Arsenal

Speak Your Mind

*