Tetesi za usajili Arsenal-Lucas Torreira-Benjamin Pavard-Steven N’Zonzi

Leo katika tetesi za usajili Arsenal tunakuletea habari zilizoandikwa na magazeti mbali mbali kuhusu wachezaji wanaohusishwa kuhama ama kuhamia Arsenal.Katika tetesi za leo tunaangalia wachezaji watatu ambao ni Lucas Torreira,Benjamin Pavard,Steven N’Zonzi.

Lucas Torreira

Tetesi za usajili Arsenal-Lucas Torreira-Benjamin Pavard-Steven N’Zonzi

Lucas Torreira

Vyombo vingi za habari vinahabarisha ya kwamba usajili wa Lucas Torreira kwenda Arsenal umeshakamilika kwa asilimia kubwa.Gazeti la Express linaandika ya kwamba baba mzazi wa mchezaji huyo amedhibitisha ya kwamba mwanaye atafanya vipimo vya afya Arsenal mara baada ya kumalizika kwa kombe la dunia linaloendelea nchini Urusi.

Benjamin Pavard

Tetesi za usajili Arsenal-Lucas Torreira-Benjamin Pavard-Steven N’Zonzi

Benjamin Pavard

Jana kulikiwa na tetesi za kwamba Arsenal ilikuwa inamtaka beki huyo wa kifaransa, anayeichezea timu ya Stuttgart  ya Ujerumani.

Lakini gazeti za Metro linaandika ya kwamba timu ya Stuttgart, haipo tayari kumuuza mchezaji huyo katika majira haya ya usajili,lakini wapo tayari kufanya dili ambalo litamuwezesha kuhama katika usajili wa msimu ujao.

Pavard amepata umaarufu mkubwa baada ya kufunga bonge la goli katika mchezo wa kombe la dunia kati ya Ufaransa na Argentina.

Steven N’Zonzi

Gazeti la Sun, linaandika ya kwamba mchezaji huyo wa Sevilla ambaye kwa sasa yupo na timu ya taifa ya Ufaransa inayoshiriki kombe la dunia nchini Russia amewasilisha rasmi ombi la kuihama timu hiyo na wakati huohuo kukiwa na taarifa za kwamba Arsenal imepeleka ombi la kumsajili mchezaji huyo kwa dau la paundi milioni 15, ombi ambalo limekataliwa na Sevilla.

Hizi ndizo tetesi za usajili wa Arsenal nilizokuandalia kwa siku ya leo, usikose kuutembelea ukurasa huu kwa ajili ya kupata tetesi kama hizi na habari nyingine kuhusu Arsenal.

Pia kumbuka kushare habari hizi na mashabiki wengine wa Arsenal.

 

Speak Your Mind

*