Tetesi za usajili-Arsenal wanamfukuzia Barella

Arsenal imeingia katika mbio za kumuwania kiungo wa Cagliari, Nicolò Barella na wapo tayari kulipa dau la paundi milioni 50 ili kumpata kiungo huyo.

Tetesi za usajili-Arsenal wanamfukuzia  Barella

Mtandao wa football Italia unaandika ya kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye aliichezea timu ya taifa ya Italia kwa mara ya kwanza wiki iliyopita wakati Italia ilipotoka sare ya 1-1 na Ukraine kwa sasa yupo katika rada za Arsenal.

Mchezaji huyo tayari amehusishwa na kuhamia timu za Milan, Inter, Juventus, Roma, Napoli, Liverpool na Chelsea, na sasa inadaiwa ya kwamba Arsenal wapo tayari kujaribu kumsajili mchezaji huyo na hawataogopa dau la paundi milioni 5o linalotakiwa na timu yake ili wamuachie.

Barella ni mmoja ya wachezaji wanaotajwa kuja kujaza nafasi inayotegemewa kuachwa na Aaron Ramsey ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

 

Speak Your Mind

*