Tetesi za usajili Arsenal-Yann Sommer-Kingsley Coman-Ospina na Akpom

Wakati Arsenal kesho ikitegemewa kusafiri kuelekea Singapore kwa ajili ya michezo ya kirafiki,Vyombo vingi vya habari vimeendelea kuihusisha Arsenal na usajili wa wachezaji mbalimbali.Katika tetesi za usajili wa Arsenal leo tunakuletea taarifa kuhusu Yann Sommer,Kingsley Coman, David Ospina na Chuba Akpom.

Yann Sommer

Yann Sommer

Yann Sommer yupo katika mazungumzo na Arsenal

Gazeti la Marca linaandika ya kwamba Arsenal wapo katika mazungumzo ya kumsajili golikipa kutoka Uswisi,Yann Sommer.

Habari hizo zinakuja huku tayari Arsenal ikiwa imeshamsajili Bernd Leno kwa dau la paundi milioni 19, huku ikiwa na makipa wengine watatu.Martinez,Ospina na Cech.

Sioni Arsenal ikisajili kipa mwingine labda Ospina na Cech wauzwe, pia Barcelona inasemekana inataka kumsajili golikipa huyo wa kimataifa wa Uswisi.

Kingsley Coman

Inasemekana ya kwamba Arsenal ipo sokoni kutafuta winga mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kukokota mpira,na jina la Kingsley Coman, linaendelea kutajwa.Vyombo vingi vya habari vinadai ya kwamba tayari Arsenal imetuma ofa mbili za kumsajili mchezaji huyo lakini zote zilikataliwa na timu yake ya Bayern Munich.

David Ospina

Inavyoonekana ni kwamba siku za David Ospina kuwa golikipa wa Arsenal zimefikia ukingoni,magazeti mengi ya kiingeleza yanahabarisha ya kwamba anakaribia kutua Besiktas, huku pia kukiwa na taarifa ya kwamba timu za Fulham na Tigres ya Mexico zinamuwania golikipa huyo.

Chuba Akpom

Mshambuliaji wa Arsenal, Chuba Akpom yupo karibu na kujiunga na timu ya Sint-Truiden ya Ubelgiji kwa dau la uhamisho linalokadiliwa kufikia paundi milioni 2.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Nigeria ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal, na hayupo katika kikosi cha Arsenal kinachosafiri kesho kuelekea Singapore.

Baada ya kuchezea timu nyingi kwa mkopo inaonekana kwa sasa Arsenal wanampango wa kuachana naye moja kwa moja.

Hizo ndizo tetesi za usajili wa Arsenal tulizopata kwa siku ya leo, zingine tukijaaliwa.

Speak Your Mind

*