Tetesi za usajili arsenal-Yannick Carrasco,Ever Banega na Denis Suarez

Wakati dirisha la usajilila majira ya kiangazi likikamilisha wiki yake ya kwanza Arsenal imeendelea kuhusishwa na usajili wa wachezaji mbali mbali.

Leo katika tetesi za usajili za Arsenal tunakuletea taaria za wachezaji watatu ambao wametawala vyombo vya habari katika siku ya leo wachezaji hao ni Yannick Carrasco,Ever Banega na Denis Suarez.

Yannick Carrasco

Tetesi za usajili arsenal-Yannick Carrasco,Ever Banega na Denis Suarez

Mtandao wa SkySport Italia unaripoti ya kwamba Arsenal inaongoza mbio za kumsajili mchezaji wa Yannick Carrasco kutoka katika timu ya Dalian Yifang inayoshiriki super league ya China.

Mchezaji huyo ambaye aliwashangaza mashabiki wengi wa soka kwa kuamua kuhamia timu hiyo ya china mwezi wa pili mwaka jana inasemekana ameshindwa kuendana na maisha ya China na sasa anataka kurudi ulaya.

Timu za Machester United na AC Milan zinatajwa kumuhitaji mchezaji huyo ingawa taarifa hiyo ya SkySport Italia inadai ya kwamba mchezaji huyo anapenda kujiunga na timu ya Arsenal.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaweza kupatikana kwa dau ya paundi milioni 20 na kwa sasa anapata mshahara wa paundi 154,000 kwa wiki.

Denis Suarez akaribia kutua Arsenal

Mwandishi wa kituo cha SkySport, Dharmesh Sheth ameandika leo ya kwamba Arsenal ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kiungo Denis Suarez kutoka Barcelona.

Suarez ambaye alicheza chini ya Unai Emery akiwa na timu ya Sevilla, jana alikosa mchezo kati ya Barcelona na Getafe licha ya kusafiri na timu.

Ever Banega

Ever Banega

Ever Banega

Gazeti za The Mirror linaandika ya kwamba bodi ya Arsenal imeingilia kati na kumzuia kocha wa Arsenal kumsajili kiungo Ever Banega.

Kiungo huyo ambaye alikuwa ni sehemu kubwa ya mafanikio ya Unai Emery akiwa na timu za Valencia na Sevilla ambapo wawili hao walifanikiwa kubeba kombe la Europa Ligi alihusishwa na kuhamia timu ya Arsenal katika majira haya ya usajili.

Lakini taarifa mpya ni kwamba bodi ya Arsenal imetupilia mbali mpango huo wa Emery kwa sababu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ni ghali na pia umri umemtupa mkono, hivyo ameambiwa atafute mchezaji ambaye ni kijana.

Hii ndiyo sababu ya Arsenal kutaka kumsajili Denis Suarez ambaye ana miaka 25 na anahitaji pesa kidogo ili kuweza kusajiliwa.

Hizo ndizo tetesi kubwa za usajili wa Arsenal kwa siku ya leo, Mungu akipenda, kesho tutakuletea tetesi nyingine .

Comments

  1. tunaitaji arsenal kusajili wa chezaji wenye kiwango kikubwa.

Speak Your Mind

*