Unai Emery abeba jeshi zima kuelekea Baku

Arsenal wapo katika mji wa Baku nchini Azerbaijan, wakijiandaa kupambana na Qarabag ya nchini humo, kuelekea katika mchezo wa makundi wa kugombea kombe la Ueropa League.

Unai Emery abeba jeshi zima kuelekea Baku

Arsenal wakifanya mazoezi mjini baku

Tumezoea kuona timu kubwa zikipumzisha wachezaji wake muhimu katika mechi kama hizi lakini naona ya kwamba Emery yeye ameamua kuweka msisitizo na kupekeka kikosi chote kwa kwanza.

Katika picha zilizowekwa mtandaoni na Ukurasa rasmi wa Arsenal, zilionesha wachezaji wote wa kikosi cha kwanza ambao wapo fiti wakipanda ndege kuelekea nchini Azerbaijan.

Ukiondoa wachezaji walio majeruhi kama Petr Cech na Laurent Koscienly, Emery aliawaacha Uingeleza wachezaji watatu tu wa kikosi cha kwana.

Wachezaji walioachwa ni Aaron Ramsey ambaye anategemewa kupata mtoto siku si nyingi, Pierre Emerick Aubamayang ambaye hadi juzi alikuwa anaumwa homa na Henriki Mkhitaryan ambaye hakuweza kusafiri kutokana na uhusiano wa kidipromasia kati ya Armenia na Azerbaijan kuwa na matatizo.

Kwa hali inavyoonesha inawezekana leo tutaona Arsenal ikipanga kikosi chake cha kwanza ili kujihakikishia ushindi katika mchezo huo.

Hapa chini ni video ya wachezaji wa Arsenal wakifanya mazoezi mjini Baku, usikose kuangalia goli la Özil.

 

Speak Your Mind

*