Unai Emery apata ushindi wa kwanza Arsenal ikiifunga West ham 3-1

Unai Emery amepata ushindi wake wa kwanza kama kocha mkuu wa Arsenal baada ya washika bunduki wa Arsenal kuishinda timu ya West Ham kwa jumla ya magoli 3-1.

Unai Emery apata ushindi wa kwanza Arsenal ikiifunga West ham 3-1

 

Magoli kutoka kwa Nacho Monreal, goli la kujifunga na Issa Diop na goli la dakika za mwisho kutoka kwa Danny Welbeck yalitosha kuipatia ushindi Arsenal baada ya Marko Arnautovic kuipatia timu ya West Ham goli la kuongoza katika dakika ya 25.

Dakika tano baada ya goli la Arnautovic, Monreal aliisawazishia Arsenal baada ya kupiga shuti kali kutoka mita kama nae hivi baada ya golikipa wa West Ham Lukasz Fabianski,kuutema mpira ambao ulimkuta mfungaji.Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Arsenal 1-1 West Ham

Kipindi cha pili kilianza kwa Unai Emery kumtoa Alex Iwobi na kumuingiza Alexander Lacazette na mabadiliko hayo yalionekana kuinufaisha Arsenal kwani ilianza kushambulia mara kwa mara.

Arsenal walipata bao la kuongoza baada ya beki Diop kujifunga kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na mshambuliaji wa Arsenal,Alexander Lacazette.

Alikuwa na mshabuliaji Danny Welbeck aliyeihakikishia Arsenal pointi tatu muhimu baada ya kupokea krosi safi iliyopigwa na beki wa Arsenal,Hector Bellerin.

Hadi mwisho wa mchezo huo,Arsenal 3-1 West Ham.

Ushindi huo umekuja wakati mzuri hasa ukizingatia ya kwamba Arsenal ilifungwa katika michezo yake miwili ya mwanzo dhidi ya Manchester City na Chelsea.

Hapo chini nimeweka magoli yote kwa wale ambao hawakuyaona au wale ambao wanataka wayaangalie kwa mara nyingine.

Speak Your Mind

*