Vijana wa Freddie Ljungberg wafanya mazoezi ya timu ya wakubwa

Pamoja ya kwamba wachezaji wengi wa Arsenal wameondoka na kwenda kujiunga na timu zao za taifa ,Arsenal jana iliendelea na mazoezi katika viwanja vya London Colney.

Vijana wa Freddie Ljungberg wafanya mazoezi ya timu yaa wakubwa

Rob Holding akiwa na Hector Bellerin katika viwanja vya London Colney

Katika mazoezi hayo yaliyoongozwa na kocha mkuu Unai Emery akisaidiwa na kocha wa timu ya vijana ya Arsenal mkongwe Freddie Ljungberg, pia yaliwajuuisha baadhi ya wachezaji  kutoka katika kikosi cha vijana wenye umri wa miaka 23.

James Olayinka, Tolaji Bola, Charlie Gilmour, Julio Pleguezuelo, Joseph Olowu, Tobi Omole, Zech Medley, Nathan Tormey na Dominic Thompson walifanya mazoezi ya timu ya wakubwa.

Wachezaji wa kikosi cha kwanza waliofanya mazoezi hapo jana ni  Emiliano Martinez, Nacho Monreal, Shkodran Mustafi, Hector Bellerin, Sead Kolasinac, Alex Lacazette, Carl Jenkinson, Stephan Lichtsteiner na Rob Holding. Laurent Koscielny alifanya mazoezi mepesi.

Wachezaji wa Arsenal walioenda katika timu zao za taifa ni Bernd Leno, Danny Welbeck, Aaron Ramsey, Lucas Torreira, Henrikh Mkhitaryan, Granit Xhaka, Sokratis, Pierre-Emerick Aubameyang, Alex Iwobi na Mohamed Elneny .

Wachezaji ambao walikosa mazoezi kutokana na bado kuwa majeruhi ni  Mesut Ozil, Petr Cech, Ainsley Maitland-Niles na Konstantinos Mavropanos .

Baadhi ya wachezaji wa timu ya vijana chini ya miaka 23 walioitwa kwenye timu zao za taifa ni Eddie Nketiah, Joe Willock, Robbie Burton, Tyreece John-Jules, Arthur Okonkwo na Bukayo Saka.

Mechi inayofuata ya Arsenal itakuwa dhidi ya Leicester City jumatatu ya tarehe 22 ya mwezi huu.

Speak Your Mind

*