Vorskla Vs Arsenal-Emery abeba watoto kibao

Vorskla Vs Arsenal-Emery abeba watoto kibao

Wachezaji waliosafiri kwenda kiev kucheza na Vorskla

Tangu nianze kushabikia Arsenal sijawahi kuona mchezo uliogubikwa na utata mwingi kama huu wa leo kati ya Vorskla na Arsenal.

Kutokana na hali ya usalama kutokuwa nzuri shirikisho la soka la Ulaya UEFA liliamua kuubadilisha mchezo huo kutoka Poltava na kwenda Kiev kwa sababu za kiusalama.

Kuna mashabiki wengi wa Arsenal ninaowafahamu tayari walishasafiri kwenda Poltava na wengine tayari walishalipia tiketi za ndege kwenda huko pamoja na gharama za hoteli.

Kubadilika kwa uwanja kutawafanya kutumia pesa nyingi zaidi ya walizotarajia pia baada ya Uefa kutangaza mabadiliko hayo timu ya Vorskla ilionesha kutokufurahishwa nayo na kutishia kutokupeleka timu uwanjani.

Pamoja na matatizo yote hayo timu ya Arsenal ikiongozwa na kocha mkuu Unai Emery ilifika Kiev jana jioni ambapo Emery alikagua uwanja wakapasha misuli na kurudi hotelini kupumzika.

Kutokana na ratiba kuwa ngumu (Arsenal itacheza na Totenham jumapili na Jumatano ijayo itacheza na Manchester United), Emery aliamua kwenda Kiev na kikosi kinachoundwa na wachezaji wengi vijana.

Katika wachezaji hao walioenda 12 wanatoka katika chuo cha soka cha Arsenal, huku wengi wao wakitarajiwa kushiriki katika mchezo wa leo.

Arsenal tayari wameshafuzu kwa hatua ya mtoano wa michuano hii na ushindi wowote leo unawahakikishia kushika nafasi ya kwanza kwenye kundi.

Kingine nilichoona kwenye kikosi hicho ni kwamba Arsenal imesafiri na mabeki wa kati wawili tu, Rob Holding na kinda mwenye umri wa miaka 18 Zech Medley.

Kama ataamua kutokumuanzisha Medley anaweza akaanza na Julio Pezquelo ambaye ni beki wa kushoto ingawa anaweza kucheza kama beki wa kati, ama mmojawapo katika ya Carl Jenkinson au Stephan Lichtsteiner, pia Mohamed Elneny anaweza kucheza kama beki wa kati.

Arsenal bado wana mchezo mmoja mkononi dhidi ya Qarabag utakaochezwa katika uwanja wa Emirates ambapo Emery ataweza kutumia wachezaji wakongwe hivyo leo anaweza akapanga madogo wote ili wapate uzoefu kwani hata kama wakifungwa matokeo hayataleta madhara yeyote kwa Arsenal.

Kila la heri Arsenal

#COYG

Speak Your Mind

*