Wachezaji waliobaki Arsenal baada ya Dirisha la usajili kufungwa

Jana dirisha la usajili kwa timu za kiingeleza lilifungwa rasmi,na kama kawaida Arsenal ilikuwa inahangaika kusajili baadhi ya wachezaji na pia kuuza baadhi ya wachezaji.

Wachezaji waliobaki Arsenal baada ya Dirisha la usajili kufungwa

Kwa jana mchezaji pekee wa Arsenal aliyefanikiwa kuhama ni Lucas Pérez, ambaye alihamia West ham,Kuondoka kwa mchezaji huyo kulifanya idadi ya wachezaji wasio wazawa kufikia 17, kiasi ambacho kisheria ndicho kinachotakiwa.

Mchezaji mzawa ni yule mchezaji ambaye amecheza katika timu iliyochini ya chama cha soka cha Uingeleza au Wales kwa miezi 36 kabla ya kufikisha umri wa miaka 21.

Timu zinaruhusiwa kutumia idadi yeyote ya wachezaji wasiozidi miaka 21 na wachezaji wasio wazawa wenye umri wa zaidi ya miaka 21 wanatakiwa wasizidi 17.

Baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili  ifuatayo ni orodha ya wachezaji wenye umri wa zaidi ya miaka 21  waliobaki Arsenal.

Jina Nafasi Mzawa       Zaidi ya miaka 21
1 Aaron Ramsey Kiungo Ndiyo Ndiyo
2 Alex Iwobi Kiungo Mshambuliaji Ndiyo Ndiyo
3 *Carl Jenkinson Beki wa Kulia Ndiyo Ndiyo
4 Cohen Bramall Beki wa kushoto Ndiyo Ndiyo
5 Danny Welbeck Mshambuliaji Ndiyo Ndiyo
6 Deyan Iliev Golikipa Ndiyo Ndiyo
7 Emiliano Martinez Golikipa Ndiyo Ndiyo
8 Hector Bellerin Beki wa kushoto Ndiyo Ndiyo
9 Rob Holding Beki wa kati Ndiyo Ndiyo
1 Andre Lacazette Mshambuliaji Hapana Ndiyo
2 Bernd Leno Golikipa Hapana Ndiyo
3 *David Ospina Golikipa Hapana Ndiyo
4 Granit Xhaka Kiungo wa kati Hapana Ndiyo
5 Henrikh Mkhitarian Kiungo mshambuliaji Hapana Ndiyo
6 *Joel Campbell Mshambuliaji Hapana Ndiyo
7 Laurent Koscielny Beki wa kati Hapana Ndiyo
8 Lucas Torreira Kiungo mkabaji Hapana Ndiyo
9 Mesut Özil Kiungo Mshambuliaji Hapana Ndiyo
10 Mohamed Elneny Kiungo wa kati Hapana Ndiyo
11 Nacho Monreal Beki wa kushoto Hapana Ndiyo
12 Petr Cech Golikipa Hapana Ndiyo
13 Pierre-Emerick Aubameyang Mshambuliaji Hapana Ndiyo
14 Sead Kolasinac Beki wa Kushoto Hapana Ndiyo
15 Shkodran Mustafi Beki wa kati Hapana Ndiyo
16 Sokratis Papastathopoulos Beki wa kati Hapana Ndiyo
17 Stephan Lichtsteiner Beki wa kulia Hapana Ndiyo

Ukiangalia vizuri kuna wachezaji 17 wenye umri wa zaidi ya miaka 21, kocha mkuu wa Arsenal alisema ya kwamba wachezaji Carl Jenkinson, David Ospina na Joel Campbell wanaweza kuondoka kabla ya dirisha la usajili la Ulaya halijafungwa.(dirisha la usajili la ulaya linafungwa tarehe 31 ya mwezi huu) Hapo utaona ya kwamba bado kuna nafasi ya kusajili wachezaji wasio wazawa na wenye umri wa miaka 21.

Kuongeza kwa orodha hiyo, kuna wachezaji ambao wana umri wa chini ya miaka 21

Jina Nafasi Atakuwa mchezaji mzawa akifikisha miaka zaidi ya 21
1 Ainsley Maitland-Niles Kiungo/Beki wa kushoto Ndiyo
2 Edward Nketiah Mshambuliaji Ndiyo
3 Emile Smith-Rowe Kiungo mshambuliaji Ndiyo
4 Joe Willock Kiungo wa kati Ndiyo
5 Joshua DaSilva Mshambuliaji Ndiyo
6 Reiss Nelson Kiungo mshambuliaji Ndiyo
7 Konstantinos Mavopranos Beki wa kati Hapana
8 Matteo Guendouzi Kiungo mkabaji Hapana

Hiyo ni orodha ya wachezaji ambao watakua katika kikosi cha kwanza, lakini ikumbukwe ya kwamba wachezaji wote chini ya umri wa miaka 21 wanaruhusiwa kucheza katika timu ya wakubwa bila hata kuwa katika orodha ya awali.

Ifuatayo ni Orodha ya Wachezaji wapya

Waliojiunga na Arsenal: Jumla 5

 • Lucas Torreira Sampdoria, £26.5m
 • Bernd Leno Leverkusen, £19.2m
 • Sokratis Papastathopoulos Dortmund, £17.7m
 • Matteo Guendouzi Lorient, £8m
 • Stephan Lichtsteiner Juventus,bure.

Walioondoka: Jumla  10

 • Lucas Pérez West Ham, £4m
 • Jeff Reiné-Adelaïde Angers, £2.7m
 • Chuba Akpom PAOK, £900,000
 • João Virginia Everton, Haijuikani
 • Jack WilshereWest Ham, Bure
 • Santi Cazorla Villarreal, Bure
 • Hugo Keto Brighton,Bure
 • Calum Chambers Fulham, Mkopo
 • Takuma Asano Hannover, Mkopo.
 • Per Metersacker , Amestaafu

Tofauti kati ya pesa ya kunununa na kuuza wachezaji: £63.8m

Hicho ni kikosi kamili cha Arsenal baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili, maoni yako kuhusu nafasi ya kikosi hiki katika msimu mpya wa ligi?

Comments

 1. Huyo beki 2 wa arsenal hector mmekosea hapo sio mzawa hebu angalieni vizuri.

  • Mchezaji mzawa ni yule ambaye amecheza soka katika timu ya Uingeleza au Wales kwa miezi 36 kabla ya kufikisha umri wa miaka 21, Hector Bellerin kisheria ni mzawa kwani alikuja Arsenal akiwa na miaka 16.
   Tunaposema mzawa hatumaanishi ya kwamba alizaliwa Uingeleza, tunamaanisha alichezea timu ya Kiingeleza kwa muda usiopungua miaka mitatu kabla hajatimiza miaka 21.

Speak Your Mind

*